Friday, 28 July 2017

BAADHI YA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO

Tags















WASOMALI WAMPONZA KIGOGO WA UHAMIAJI

Tags
Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume cha taratibu.

Kauli hiyo imetolewa  jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.

Alisema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.

"Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu." alisema Waziri Mkuu

Waziri Mkuu alisema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini

 "Tulidhani ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari hatuwezi  kuivumilia. Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao" alisisitiza Majaliwa

TAHADHARI!HOMA YA INI

Tags


Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia  Wazee na Watoto.kitengo cha elimu kwa umma imewataadharisha wananchi juu ya Homa ya ini(Hepatitis)

Katika tangazo hilo limetoa jinzi ya kujikinga na homa na ini ikiwa ni pamoja na,Kuepuka kuchangia sindano na vitu vyenye ncha kali.Kutumia kinga(Condom)kwa usahihi unapojamiiana,kuepuka kujidunga madawa ya kulevya,na kupata chanjo ya homa ya ini.

Pia ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya mate na jasho.

TAFADHARI:fika vituo vya afya kwa ajili ya kinga ya ugonjwa huu

DANGOTE ASHUKA NAFASI ZA WATU TAJIRI DUNIANI

Tags








Bilionea raia wa Nigeria Aliko Dangote ameporomoka kwenye nafasi za watu tajiri duniani hadi 105 kutoka nafasi ya 51. 

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes limeripoti kwamba utajiri wa Dangote umepungua kutoka dola bilioni 15.4 mwaka 2016 hadi dola bilioni 12.2 mwaka huu kutokana na kushuka thamani kwa pesa ya Nigeria.

 Dangote alijipatia utajiri wake kupitia uzalishaji wa saruji, sukari, na unga wa ngano. Aligonga vichwa vya habari 2016 wakati aliposema kuwa alitaka kuinunua klabu ya soka ya Arsenal katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Pamoja na bishara hizo Dangote pia ana viwanda nchi kadhaa za Afrika kikiwepo cha Dangote Cement kilichopo mkoani Mtwara,kilichozinduliwa na Rais Dr John Pombe Magufuli mapema mwaka huu.

Hapo juzi  Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos alimpiku Bill Gates kwa muda mfupi kama mtu tajiri duniani kabla ya kushuka hadi nafasi ya pili.

kurunzi huru blog ipo hewani karibuni

Tags
Karibu kwenye blog yako pendwa ya kurunzihuru.blogspot.com Hapa utapata habari za kitaifa na kimataifa. Utapata habari za michezo za burudani na habari nyinginezo,. Zaidi ya kupata habari utapata makala za kijamii makala zinazofundisha mambo mbalimbali ya kimaisha hii ni sababu kuu ya wewe kuitembelea blog hii kila siku kupata elimu ya kuboresha maisha yako


Ukiwa na matangazo unakaribishwa kutangaza kwenye blog hii kwa bei nafuu sana. Wasiliana nasi kwa email yetu hii braimmedia@gmail.com sio brainmedia@gmail.com hapana tumia email hiyo ya kwanza.

Saidia kushare blog hii facebook kwenye magroup uliyojiunga share whatsapp kwenye magroup uliyojiunga Adika anwani ya blog hii ambayo ni kurunzihuru.blogspot.com mtu yoyote huko whatsapp akibonyeza anwani hiyo ataletwa hapa kupata mambomazuri pamoja nawe. Ukiwa na swali au maoni uliza hapa chini kwenye comment section. Karibu sana